- Dar sasa majimbo 8, mapya ni Chamazi na Kivule -Wabunge kuongezeka Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, (INEC), imetangaza majimbo mapya nane ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu ujao wa madiwani, wabunge na Rais, huku ikibadili majina ya majimbo tisa. Mwenyekiti wa INEC,Jaji wa Rufaa, J acob's C Mo Mwambegele Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa leo na tume hiyo, mikoa ya Dar es Salaam na Geita imefadiika zaidi kwa kuongezewa majimbo mawili kila mmoja, ambapo Dar es Salaam majimbo mapya ni Chamazi na Kivule, huku Geita mapya yakiwa Katoro na Chato Kusini. Kufuatia mabadiliko hayo, Dar sasa itakuwa na majimbo nane kutoka sita ya awali ambayo ni Ilala, Kinononi, Mbagala, Temeke, Ubungo na Kibamba, Chamazi (jipya) na Kivule (jipya). Geita pia itakuwa na majimbo nane ambayo ni Chato Kusini, Chato Kaskazini, Katoro, Butundwe, Busanda, Nyang’wale, Mbogwe na Bukombe. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa, J acob's C Mo M...