Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Fuso lilipakia viroba 83 vya bangi-Korti yaelezwa

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

SHAHIDI wa Jamhuri ASP Njama amedai Fuso lililobeba mikungu ya ndizi 80 (pichani) chini lilipakia viroba 83 vya bangi.





Alidai Fuso hilo walilokuwa wanalisaka lilitokea Mkoa wa Mara  lilipata  ajali maeneo ya Chamakweza wilayani Chalinze wakalikamata.

ASP Njama amedai hayo Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi mbele ya Jaji Godfrey Isaya wakati anatoa ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mshtakiwa katika kesi hiyo, Raisan Mussa anashtakiwa kwa kukutwa na viroba 83 vyenye majani yanayosadikiwa dawa za kulevya aina ya bangi.

Amedai walikuta Fuso lenye namba T223 ATC limepata ajali maeneo ya Chamakweza Chalinze wakatilia shaka kwa kuwa walikuwa na taarifa kutoka kwa msiri kuhusu gari hilo.

Shahidi amedai walianza kupekua na baada ya dakika chache, Koplo George alisema juu kuna ndizi lakini chini kuna viroba vya mifuko ya salfeti akaamuru ndizi za juu zitolewe, zilishushwa zote,  ilikuwa mikungu 80.

Mikungu ya ndizi ilishushwa, eneo la chini gari lote lilijaa viroba vya salfeti, aliwaamuru vishushwe, wakakagua kiroba kimoja wapo wakakuta majani makavu yadhaniwayo kuwa dawa za kulevya lakini kwa harufu ilikuwa bangi 

Anadai Koplo George alitoa majani kidogo kuangalia ikaonekana ni bangi aliamuru mifuko yote ya salfeti ishushwe chini na wakati vinashushwa vilikutwa viroba 83 vyenye majani makavu yadhaniwayo kuwa dawa za kulevya.

Mahakamani ilihamia nje kwa ajili ya kutambua Fuso hilo na shahidi alilitambua.

Chapisha Maoni

0 Maoni