![]() |
Dudley Mbowe |
Wadai ambao ni Maregesi Paul na wenzake 9 waliwasilisha maombi mahakamani hapo ya kumkamata Dudley na kumtupa gerezani kama mfungwa wa kiraia baada ya kushinda tuzo ambayo Dudley hakuitekeleza.
Januari 14 mwaka huu mahakama hiyo ilimuonya Dudley mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Mary Mrio akielezwa hajawahi kufika mahakama licha ya kuahidi kufanya hivyo, huku akiamriwa kufika mahakamani na kulipa malimbikizo hayo kabla ya Januari 31,2025.
Siku hiyo,
Wakili Samadani Mngumi aliyemwakilisha Dudley mahakamani, alidai mbele ya Msajili Mrio kwamba alikuwa hajazungumza na mteja wake zaidi ya kupokea maelekezo ya kufika mahakamani kuomba udhuru.
Awali Mahakama hiyo ilitoa amri ya waandishi hao kulipwa baada ya kupitia hoja za washinda tuzo katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Julai 2023.
Shauri hilo namba 28461 la mwaka 2023, wadai Maregesi Paul na wenzake tisa dhidi ya Mkurugenzi wa Gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe.
Maregesi nawenzake 9 walipata tuzo Julai 17 mwaka 2023 mbele ya Msuluhidhi wa CMA Ilala, Bonasia Mollel.
Madai ya awali yalikuwa jumla ya Sh, milioni 114.lakini baada ya kukaa mezani kwa majadiliano, kiwango hicho cha fedha kilishuka na kufikia Sh. milioni 62.7.
Mkurugenzi wa Tanzania Daima (Dudley), alikubali kulipa fedha hizo kwa awamu tatu, Oktoba 30, Desemba 30 mwaka 2023 na awamu ya mwisho ilikuwa mwishoni Februari mwaka jana, hata hivyo hakulipa.
Dudley aliingia makubaliano ya kulipa malimbikizo hayo nje ya Mahakama Aprili hadi Mei mwaka jana, lakini pia hajafanya hivyo.
0 Maoni