Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Tanzania Women Tapo, Aga Khan wazindua Kampeni ya Afya kwa Wanawake

 -'Wamwita' Rais Samia


Na HusseinNdubikile, daimatznews@gmail.com

Shirika la Tanzania Women Tapo kwa kushirikiana na Hospitali ya Aga Khan wamezindua rasmi Kampeni ya Afya kwa Wanawake wa Masokoni na Wachuuzi, mpango unaolenga kuwafikia wanawake 31,000 katika mikoa yote 31 ya Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Women Tap,Lulu Nyapili, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Desemba 5, 2024.

Akizungumza  jijini humo wakati wa  uzinduzi  uliofanyika  Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam leo Desemba 5,2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Women Tap,Lulu Nyapili,amesema  kampeni hiyo inalenga kutoa huduma za uchunguzi wa afya, elimu ya kifedha na uhamasishaji wa masuala ya kijamii kwa wanawake wa masokoni na wachuuzi,wanaotajwa kuwa mhimili muhimu wa uchumi wa taifa.

“Hawa si wauzaji tu, bali ni wajasiriamali, mama na viongozi wa jamii. Kampeni hii siyo tu mpango wa afya, bali ni matumaini na mabadiliko,” amesema.

Nyapili amebainisha kuwa changamoto nyingi zinazowakabili wanawake huku juhudi zinaendelea kuhakikisha wanapata heshima na msaada wanaostahili.

“Wanawake hawa wanahitaji kuonekana, kusikika, na kuthaminiwa,” ameongeza.
Mkurugenzi huyo amemwomba Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kushiriki katika kampeni hiyo na kukutana na wanawake hao ili kusikiliza changamoto na ndoto zao.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mganga Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Ayoub Kibao,ambaye pia ni Mratibu wa Huduma za Ukimwi mkoani humo, amesema Serikali inatambua mchango wa Afya wanawake kwani bila afya ya wanawake Taifa haliwezi kupiga hatua.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Huduma Afya Aga Khan,Sisawo Konteh,amesema makubaliano na taasisi  hizo yanalenga kuwasaidia wanawake wa kitanzania kimatibabu.

Chapisha Maoni

0 Maoni