YANGA YAMTIMUA KOCHA

Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com

Siku tatu baada ya kucheza Dabi ya Kariakoo na kutoka sare mtani wake Simba kwa kufungana magoli 2-2, Klabu ya Yanga imetangaza kumfukuza kazi kocha wake mkuu wa kikosi cha kwanza,Pedro Gonçalves.

Ikumbukwe kuwa Dabi ya Kariakoo ilichezwa Mei 3, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo, Mbweni Dar es Salaam ikiwa ya mkondo wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwenyeji akiwa Simba.

Yanga imemkabidhi Abdihamid Moalin mikoba ya Pedro.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga leo Mei 6, 2026 imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya tathmini ya ndani.

Yanga imeshukuru kocha huyo kwa mchango wake ndani ya klabu hiyo na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake yajayo.

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi