Waziri wa Maini atangazia kiama kampuni 95 za madini
▪️Yatoa hati za makosa kwa kukiuka masharti ya Leseni
▪️Kampuni 7 ambazo hazijaanza uchimbaji zimelaza mtaji wa Sh.trilion 15
▪️Zapewa siku 30 kujibu hoja
![]() |
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mei 6,2025 |
Akizungumza leo Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema kampuni hizo zinapaswa kujibu hoja ndani ya siku 30 la sivyo zitafutiwa leseni zao.
Hati hizo za makosa zimetolewa rasmi kuanzia Aprili 14, 2025 na muda wake utamalizika Mei 13 mwaka huu.
Amesema, Serikali imetoa leseni kwa wachimbaji wa kati na wakubwa ambazo tangu kutolewa kwake hazifanyiwa kazi.
Leseni 7 tu kati ya 95 ukiziweka pembeni zina mtaji wa Shilingi trilioni 15 zimelala, sisi hatuwezi kuwa nchi ambayo inatoa leseni kwa ajili ya kuchochea sekta ya madini kukua,halafu kuna watu wanachukua leseni wanakaa nazo hawafanyii kazi kwa kisingizio kuwa tupo kwenye mazungumzo na serikali na sababu mbali mbali.
Amesema na wale wote ambao wamepata hati ya makosa ambao wamejibu waende na barua ya ‘Commitment’ ya kueleza wataanza uchimbaji lini, ambao katika barua hiyo pia ikitokea ameshindwa kukidhi kile alichosema kwenye barua sheria itafuata mkondo wake.
"Wale wote ambao hawatajibu ndani ya muda uliowekwa wasitegemee huruma yoyote, na wamekuwa ni mabingwa wakukimbilia mahakamani kuishtaki serikali katika hili Serikali imefuata taratibu zote kwa mujibu wa sheria inayowataka waliopata Leseni wote kufanya uendelezaji wa Leseni zao,” amesema Mavunde.
Sekta ya Madini ni kati ya sekta zenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo shughuli za uchimbaji wa madini huchochea maendeleo makubwa ya kiuchumi
Maoni
Chapisha Maoni