Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Zaidi ya theluthi ya wananchi wa Zanzibar ni tegemezi, huku asilimia 23 ya wakazi hao wakiishi kwa kutegemea vibarua, matokeo ya utafiti wa FinScope Tanzania 2023 kwa Zanzibar yamebainisha. FinScope Tanzania ni utafiti wa kina wa mahitaji ya sekta ya fedha kwa watu wazima Tanzania, walio na umri wa kuanzia miaka 16 na kuendelea. Kwa mujibu wa matokeo hayo, katika kipengere cha vyanzo vya mapato, asilimia 17 ya Wazanzibar ni wafanyabiashara, wanaopokea mishahara ni asilimia tisa, wakulima asilimia nane na makundi mengine asilimia sita. Dk. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hali hiyo inaweza kutafsiriwa kwamba licha ya juhudi kubwa za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuendeleza wananchi wake, juhudi zaidi zinahitajia katika kupanga, kusimamia na kutekeleza mipango ya kiuchumi na maendeleo inayowahusu moja kwa moja wananchi wa Zanzibar, ili kuondokana na hali hiy...