Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Utafiti mpya wa kisayansi ubebaini kuwa mfumo wa akili bandia (AI),
una uwezo mkubwa wa kubashiri kifo cha binadamu kwa usahihi pamoja na kubainisha
hatari za kutokea vifo vya mapema.
Mfumo huo wa akili bandia uliowezeshwa na historia za mamilioni ya watu na takwimu, una kiwango kikubwa cha usahihi katika kutabiri maisha na uwezekano wa vifo kutokea kuliko mifumo yote iliyopo sasa. Wanasayansi kutoka Technical University of Denmark (DTU), wamebainisha.
Wanasayansi hao walibadili takwimu hizo kuwa katika maneno ili
kufundisha lugha ya kisayansi iitwayo “life2vec” inayoelezwa ni sawa na mifumo
ya teknolojia ya akili bandia kama ule
wa ChatGPT.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliochapichwa katika
Jarida la Nature Computational Science hivi karibuni, mara akili bandia inapofundishwa na kuelewa takwimu hizo, huzalisha mfumo bora zaidi unaoweza kuchambua kuhusu mtu binafsi na kutoa majibu yenye usahihi kwa kiwango
kikubwa cha usahihi kuonyesha muda atakaokufa.
Watafiti hao walichukua takwimu kutoka kikundi cha watu weny umri wa miaka 35 hadi 65 na nusu kati ya hao tayari wamefariki kati ya mwaka 2016 na 2020, ambapo akili bandia iliulizwa kati ya hao yupi aliye hai na aliyefariki.
Majibu ya mfumo huo wa akili bandia ulitoa majibu sahihi kwa asilimia 11 zaidi ya mifumo iliyopo sasa hata mifumo inayotumika na kampuni za bima kupanga bei na miongozo ya sera.
“ Jambo muhimu la kushangaza hapa ni maisha ya watu
kama mfululizo wa matukio, sawa na sentesi inavyoundwa na maneno yanayofuatana,”
amesema mtafiti Sune Lehman wa chuo kikuu DTU na kuongeza:
![]() |
Mtafiti, Sune Lehmann |
Hata hivyo, wanasayansi hao wameonya kuwa mfumo huo haufai
kutumika katika bima za afya kwa mujibu wa taratibu za kimaadili.
0 Maoni