Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2026

Makamu wa Rais: Uhuru wa Mahakama ni dhamana ya haki, sio kinga ya uzembe

Picha
- Mahakama zageukia AI kuongeza ufanisi utoaji haki   Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Makamu wa Rais Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua za makusudi katika kuimarisha uhuru wa Mahakama ili kuiwezesha kutekeleza wajibu wake kikamilifu na kuchochea ustawi na maendeleo ya Taifa ikitambua umuhimu wa Mahakama katika ujenzi wa Taifa. Makamu wa Rais Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi Dk. Nchimbi pia ametoa rai kwa majaji na mahakimu akitaka uhuru wa Mahakama usitumike kama sehemu ya kuficha uzembe, upendeleo au vitendo visivyo vya haki na kwamba uhuru huo ni dhamana ya kutenda haki kwa uadilifu, uwazi na kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi. Amesema hayo, alipomwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, yaliyofanyika leo Februari 2,2026 Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Tambukareli, Jijini Dodoma. “Serikali itaendelea kushirikiana na Mahakama katika ujenzi wa miundombinu ya Mahakama, kuimarisha rasili...

Nyenzo Kuu 3 Dira 2050 kuanza kuwasilishwa bungeni kesho

Picha
-Bunge kuzijadili kwa wiki nzima Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Tume ya Taifa ya Mipango inatarajia kuwasilisha Nyenzo Kuu Tatu za kuanza utekelezaji wa Dira 2050, bungeni mjini Dodoma kesho Februari 2, 2026. Katibu Mtendaji wa NPC, Dk. Fred Msemwa Baada ya kuwasilishwa na kupokelewa, Bunge litazijadili kwa muda wa wiki moja kabla ya kutoa uamuzi wake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Februari Mosi, 2026 Katibu Mtendaji wa NPC, Dk. Fred Msemwa ameeleza hayo akizitaja nyenzo hizo kuwa ni pamoja na Mpango Elekezi wa Muda Mrefu ambao ni wa miaka 25 kuanzia mwaka 2026/2027 hadi mwaka 20250/2051, Mpango Elekezi wa Miaka Mitano w mwaka 2026/2027-2030/2031 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2026/2027. “Nyenzo hizo zitawasilishwa bungeni na Serikali kupitia Waziri wa Nchi (Mipango na Uwekezaji) Profesa Kitila Mkumbo,” amesema Msemwa aliyekuwa akitoa taarifa kwa umma kuhusu maandalizi ya kuanza kwa u...