Wanyama 400 wauawa Mikumi

-Kamera kunasa wahalifu Exuperius Kachenje, daimatznews@gmail.com Hifadhi ya Taifa Mikumi inajipanga ili kuweka kamera zikazowekwa geti la kuingilia hifadhi hiyo eneo la Kijiji cha Doma, Mikumi Mjini inapoishia hifadhi kwenye barabara Kuu kwenda Iringa, inayopita hifadhini humo, ikielezwa kuwa wastani wa wanyama 400 hufa kwa kugonjwa na gari kila mwaka. Kamishna Augustine Masesa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Mikumi, Kamishna Augustine Masesa amesema hayo Juni 28/2025 akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuwanasa madereva watakaowagonga wanyama kwenye eneo la hifadhi na magari yanayovunja sheria kwa kutembea mwendo usioruhusiwa. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu hifadhi hiyo, ambapo amesema mradi huo unahitaji takriban shilingi bilioni 2. “Tayari upembuzi yakinifu umefanywa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP), tunasubiri pesa tu ipatikane kutekeleza mradi huo kwenye eneo hilo la kilometa 50 inapokatiza b...