NEEC 'yawafunda' wanawake, vijana

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), BengI Issa, amewataka wanawake na vijana kutumia vizuri na kwa nidhamu fedha zinazotolewa na taasisi za uwezeshaji, ili kasi ya kujikwamua kiuchumi iongezeke na kuleta matokeo chanya kwa fedha zinazopelekwa. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake na Vijana wa Kanisa la TAG City Light Temple, Goba, Dar es Salaam, Issa amesema Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ina nia nzuri na wazi ya kuwawezesha Watanzania kiuchumi kwa kutoa mitaji wezeshi, hasa kwa makundi maalumu kwa kutumia majukwa ya uwezeshaji. Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), BengI Issa, (kulia) akimkabidhi Taulo za Kike mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Matosa katika hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake na Vijana wa Kanisa la TAG City Light Temple, iliyofanyika jana Januari 30, 2024 Goba, j...