Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Othman Masoud Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar atafanya ziara ya kuimarisha chama hicho katika mikoa mitano ya Tanzania Bara.
![]() |
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Othman Masoud Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika moja ya mikutano yake ya kisiasa. |
Makamu huyo wa Kwanza wa Rais, atafanya ziara hiyo kuanzia Januari 14 hadi 21 katika mikoa ya Ruvuma, Mkoa wa Kichama Selous, Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es salaam.
Taarifa ya ACT Wazalendo imesema kwenye ziara hiyo, Othman Masoud atazungumza na viongozi wa majimbo yote kwenye mikoa hiyo mitano kupitia mikutano mikuu ya mikoa na kufanya shughuli nyingine za kisiasa.
0 Maoni