TTCL yaipa 'tano' DCPC

Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), limeipongeza Klabu Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC) kwa ushirikiano wa kikazi na kimkakati, iliouonyesha kwa shirika hilo kipindi chote cha mwaka 2023. Pongezi hizo zimetolewa leo Desemba 29, 2023 na Mkurugenzi wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga kupitia kwa maofisa uhusiano wa shirika hilo, Adeline Berchimance na Rehema Nyangasa waliotembelea ofisi za DCPC Mtaa wa Samora, ambapo wamewasilisha zawadi na ujumbe maalum kutoka kwa Mhandisi Ulanga, aliyesema klabu hiyo imefanya vizuri katika kuandika habari za shirika hilo na kulitangaza. Ofisa Uhusiano wa TTCL, Adeline Berchimance(Kushoto), akikabidhi zawadi maalum kwa Katibu Mkuu wa DCPC, Fatma Jalala(Kulia) pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji DCPC Bakari Matutu. Mwingine kushoto ni Rehema Nyangasa ambaye pia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, wakati ujumbe wa kampuni hiyo ulipotembelea ofisi za DCPC, Mtaa wa Samora, Dar es Salaam Desemba 29, 2023...