-Serikali yaja na mageuzi ya sheria -Wana takriban siku 200 kubaki madarakani -Mageuzi kugusa mamlaka ya Rais kuwateua -Mashirika kusajili hisa, kuongeza wajibikaji Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Siku za wakurugenzi wa mashirika ya umma na wakala za Serikali nchini zinahesabika, wakibakiwa na takriban siku 217 kabla ya kujua hatma yao, iwapo watasalia au kuondoka kwenye nafasi hizo. Kuanzia Desemba 2025, siku hizo 217 sawa na wastani wa miezi saba, zikizidishwa kwa saa 24 za kila siku moja, zinakuwa jumla ya saa 5,208 , muda unaolingana na kipindi kilichosalia kabla ya kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa ajira. Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji Hatua hiyoi inakuja baada ya Serikali kutangaza mpango wa kufanya mageuzi makubwa katika uongozi wa mashirika ya umma, unaotarajiwa kuanza rasmi Julai 1, 2026 Kwa mujibu wa Serikali, mabadiliko hayo yatakwenda na mabadiliko ya sheria ambapo Wakurugenzi wa mashirika watalazimika kuo...