Wagombea udiwani 16 Kigoma wakosa wapinzani

- Samia kunguruma Septemba 13

-Ndalichako kuwasha moto Sept 4

-Prof Yanga hapoi

Mwandishi Wetu, Kigoma

Wagombea udiwani 16 kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kigoma wamebahatika kuwania nafasi hizo bila kupingwa, baada ya vyama vingine vya siasa mkoani humo kushindwa kusimamisha wagombea, huku kwenye baadhi ya kata wagombea wa upinzani wakielezwa kukosa sifa.

Rais Dk.Samia Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, akizungumza katika moja ya mikutano yake.

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Kigoma, Deogratius Nsokolo amebainisha hali hiyo akieleza kuwa kwa CCM hiyo ni dalili njema ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao Oktoba 29, 2025, ambapo sasa wagombea hao wanasubiri kupigiwa kura za ndiyo na hapana.

Nsokolo amezitaja kata hizo ambazo wagombea wa CCM wamekosa upinzani ni pamoja na zilizopo Wilaya ya Kasulu ambapo wagombea sita waliokosa wapinzani, Wilaya ya Buhigwe kata tano, Wilaya ya Kibondo  kata nne na Uvinza ikiwa kata moja ya Basanza.

"Mchakato wa kampeni za wagombea ubunge,udiwani na  za Urais za mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan zitaendelea baada ya uzinduzi wa uliofanywa Viwanja vya Kawe jijini Dar es Salaam na kwamba Mgombea wa urais wa chama hicho atafanya mikutano ya  kampeni  mkoani humo Septema 13 mwaka huu," amesema.

Naye Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, Profesa Joyce Ndalichako amesema atazindua kampeni za majukwaani Septemba nne na kwamba michakato mingine ya kampeni itaendelea kabla ya kuanza kwa mikutano hiyo ya hadhara.

Amesema miaka mitano ambayo amehudumu nafasi hiyo ya ubunge jimboni humo kulikuwa na changamoto kubwa ya barabara za jimbo hilo na kwamba sasa tayari  barabarani nyingine zimeanza kuchongwa, sambamba na utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji, unaoendelea kutekelezwa, ambao utaondoa changanoto kubwa ya maji inayowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Buhigwe, Profesa Pius Yanda amesema baada ya uzinduzi wa kampeni uliofanywa na Mgombea uraisi wa chama hicho Agosti 28 mwaka huu,  watafanya kampeni bila kulala kuhakikisha ushindi wa wagombea wa chama hicho mwezi Oktoba mwaka huu.

Profesa Yanda amesema wakati anapambana kupata ridhaa ya wananchi kuongoza jimbo hilo, jambo la kwanza atakalolishughulikia akipewa ridhaa na wananchi kuwa mbunge ni barabara ndani ya jimbo, ambazo zitaunganisha jimbo hilo na barabara kuu ili ziweze kutafsiri kwa matendo uboreshaji wa miundo mbinu kuwezesha wakulima kuwa na barabara bora kwa usafirishaji wa mazao yao.Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi