Vigogo Kamati ya Maadili CCM 'wakesha' kuchuja wagombea
Kikao cha Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kufanyika hadi baada ya saa nane usiku wa kuamkia leo Julai 28, 2025 kupitia na kuchuja majina ya wagombea nafasi za ubunge na uwakilishi kupitia chama hicho tawala.Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM, jijini Dodoma Julai 28,2025.
Kikao hichi kimefanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma, kikijumuisha vigogo wengine wa chama hicho ambao ni wajumbe wa Kamati ya Maadili ya CCM.
Maoni
Chapisha Maoni