TAKUKURU YAWATEGA WALAJI, WATOA RUSHWA UCHAGUZI MKUU
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa
Kigoma imesema kuwa ina vyanzo vipya vya
kupata taarifa na mbinu za kisasa, itakazozitumia kudhibiti vitendo vya rushwa
katika hatua mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu katika mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Ofisa Dawati la Elimu kwa Umma TAKUKURU
Mkoa Kigoma, Abecha Bakari katika kikao kazi na waandishi wa Habari, kuweka mkakati
wa pamoja wa ushirikiano katika kufanya kazi wakati wa Uchaguzi Mkuu.
“Pamoja na mambo mengine, pia tumeongeza vyanzo vya
taarifa na namna ya kupata taarifa hizo, lakini pia na namna ya kuzifanyia kazi, hivyo tuna uhakika kuwa mwaka
huu udhibiti wa vitendo vya utoaji na upokeaji rushwa utadhibitiwa,” amesema
Bakari.
Naye Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Kigoma, John Mgallah
aliomba ushirikiano kutoka kwa waandishi wa habari mkoani humo kutumia vyombo
vyao kwa kutoa elimu kwa umma kupitia vipindi mbalimbali, kueleza madhara ya
kuchagua viongozi kwa misingi ya kupeana rushwa.
Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi
wa Habari Mkoa Kigoma, Jacob Ruvilo amesema, waandishi wa habari wako tayari
kufanya kazi na TAKUKURU na kwamba wameomba taasisi hiyo kutoa ushirikiano,
hasa taarifa za matukio ya wagombea
wanaokamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni