Maswi aipongeza Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali

Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imepongezwa kwa kuendelea kusimamia kwa weledi mashauri ya madai na usuluhishi hatua ambayo imesaidia Serikali kuongeza kasi katika kuwaletea wananchi maendeleo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakimu Maswi akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Mashauri na Uthibiti Ubora wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Mercy Kyamba alipotembelea banda la Ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi alipotembelea banda la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya 49 ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. Maswi alisema kuwa uwepo wa weledi na ufanisi katika uendeshaji wa mashauri ya madai, usuluhishi, Katiba, Haki za Binadamu na Uchaguzi katika Ofisi hiyo umeongeza kasi katika kupunguza na kutatua migogoro ya kisheria kwa njia ya majadil...