Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani
-Maajabu mapya ya kipekee Exuperius Kachenje Sanamu yenye mwonekano wa Bikira Maria (Mariam), anayetajwa na vitabu vitakatifu vya Biblia Takatifu na Qur’an Tukufu (Mariam), ndiye mama wa Yesu Kristo (Nabii Issa bin Mariam), imegundulika ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani, ikitajwa kuwa ni maajabu mapya yasiyo ya kawaida kwa watalii ndani na nje ya Tanzania, inayoongeza upekee wa hifadhi hiyo kwa utalii. Mti wa mbuyu wenye sanamu yenye mwonekano wa Bikira Maria uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadan. Picha na Exuperius Kachenje Ofisa Mhifadhi kitengo cha uta;ii, Hifadhi ya Taifa Saadani (SANAPA) Daud Gordon amebainisha hayo Juni 26, 2025 akieleza kwamba kivutio hicho kipya ni nyenzo muhimu katika kukuza utalii wa kiimani, hata kuweza kuwa sehemu ya hija kwa waamini, hasa wanaoamini na kumheshimu mama huyo kadiri ya mapokeo ya imani zao,mfano ukiwa Kanisa Katoliki. Gordon amesema kuwa sanamu hiyo ya asili inaonekana katikati ya mti wa mbuyu, eneo la Buyuni ndani ya h...
Maoni
Chapisha Maoni