Miaka minne ya Rais Dk. Samia, maagizo manne ya Msajili Hazina NHC 2025
Ndani ya muda huo, Rais Dk. Samia amefanya juhudi kuhakikisha NHC inakamilisha miradi iliyokwama tangu 2018, ambapo aliruhusu shirika hilo kukopa,hatua iliyowezesha miradi ya Kawe 711 na Morocco Square kukwamuka.
Kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dk.Samia kuifanya NHC imara zaidi imeliwezesha shirika hilo kuongeza kasi ya utendaji wake katika maeneo mbalimbali ikiwemo ubunifu hata likabuni Mradi Samia Housing Scheme, ukiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais.
Mradi huo ni wa nyumba 5,000 ambapo ujenzi wa nyumba 560 Kawe umefikia asilimia 85, ukitarajiwa kukamilika Machi 2025 na tayari nyumba hizo zimeshauzwa.
Awamu ya pili ya mradi huo inaanza Kawe zinapojengwa nyumba 500, Mdeli Dodoma nyumba 100, na Mtoni Kijichi Dar es Salaam 400.
Kwenye kipindi hicho cha miaka minne, miradi minne ya ujenzi iliyokuwa imesimama, imerejeshwa mikononi mwa NHC na kuendelea kutekelezwa,huku eneo la Kariakoo pekee likishuhudia nyumba 172 zikivunjwa kwa lengo la kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa 2,100 mpya kwa ajili ya makazi na biashara.
Katika Awamu ya Sita ya Rais Dk, Samia, Shirika Nyumba la Taifa, limepewa ukanarasi wa miradi inayofikia thamani ya shilingi bilioni 186, ikijumuisha ujenzi wa majengo ya ofisi nane za Wizara katika Mji wa Serikali wa Mtumba, Dodoma ambayo tayari imekamilishwa kwa asilimia 96.
NHC pia inajenga Shule ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ujenzi uliofikia asilimia 90, Tanzanite Building - Mirerani (asilimia 95), pia miradi ya Hospitali ya Kanda ya Kusini (Mitengo) na Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere - Musoma ambazo haisasa zilizokamilishwa kwa asilimia 100.
Mbali na hiyo, NHC pia imejenga jengo la Kitengo cha Moyo cha Jakaya Kikwete lililokamilika,huku ujenzi wa majengo ya TCRA Dodoma ukifikia asilimia 40 na Zanzibar likiwa asilimia 20.
Si hivyo tu, bali Seikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia, imeiwezesha NHC kuimarisha ushirikiano wa sekta binafsi na umma, ikiidhinisha miradi 21 ya ubia inayofikia thamani ya Shilingi Bilioni 179, huku miradi 18 tayari ikiendelea na mingine mitatu ikiwa hatua za awali.
Katika miaka minne ya utawala wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Shirika la Nyumba laTaifa (NHC), limefanikiwa kufanya mageuzi makubwa na katika sekta ya nyumba nchini, mafanikio yanayosimama kuwa ni kielelezo cha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha watanzania wanapata makazi bora hivyo kuboresha maisha yao.
Baadhi ya miradi inayoanza hivi karibuni na Shirika ni Singida 2F (Singida); Kashozi Business Center (Bukoba); Samia Housing Scheme (Kawe Awamu ya 2, Kijichi, Medeli Dodoma); Mt. Meru Plaza (Arusha); Juwata Plaza (Morogoro) na Mkwakwani Plaza (Tanga).
Miradi mingine ni Tabora Commercial Complex; Iringa ICC; Mpwapwa Flats (Dodoma); Ilala Breweries Retail Shops na Mtwara Warehouse.
Utendaji huo wa kiwango cha juu wa NHC katika miaka minne ya Rais Dk.Samia madarakani, umewezesha rasilimali za shirika hilo kufikia shilingi trilioni 5.47, zikilinganishwa na shilingi trilioni 5.04 katika mwaka 2021.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG ) ya Juni 2024 Ukuaji huu umetokana na kukamilika kwa miradi mipya na umiliki wa maeneo mapya kama Urafiki, Dar es Salaam.
Utendaji na ukuaji wa NHC umemsukuma Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu ambaye pia ni msimamizi wa mashirika yote ya umma nchini kueleza kuwa, kuimarika kwa shirika hilo kupo wazi kutokana na mizania yake kuongezeka, likiakisi pia ongezeko la asilimia 300 la uchangiaji wake kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.
Mchechu ameeleza hayo katika mahojiano nje ya ukumbi, baada ya kufungua mkutano wa Kuu la Baraza la Wafanyakazi wa NHC, uliofanyika Ukumbi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere Kibaha mkoani Pwani Februari mwishoni mwaka 2025, uliohusisha kupokea taarifa mbalimbali za kifedha, utekelezaji wa majukumu ya shirika na mikakati ya mwaka mmoja ujao Februari 24,2025.
“Cha kwanza nimeangalia utendaji wao, mizania ya shirika imeongezeka. Mwaka huu uchangiaji wao kwenye mfuko mkuu wa Serikali utaongezeka kwa asilimia 300, kutoka Shilingi Milioni 2 hadi Shilingi Milioni sita,” anasema Msajili wa Hazina nakufafanua;
“Uchangiaji huo ni nje ya kodi na makusanyo mengine wanayotoa serikalini.”
Anasema amepata fursa ya kujua miraji ya NHC inayoendelea na mipango ya miradi yao.
“Nawapa hongera kwa ukamilishaji wa miradi yenu, Mradi wa Samia unaondelea pale Kawe, ukamilishaji wa Mradi wa 711 Kawe, lakini pia ukamilishaji wa Mradi wa Premium Tower (Kawe)na 4300 ambayo ipo katika hatua za mwisho, kuhakikisha miradi hiyo iliyokwama na sasa inakamilishwa,” anasema Mchechu.
Kwa mujibu wa Mchechu, pia amepata fursa ya kujifunza miradi ya ujenzi inayoendelea kutekelezwa mikoani, ikiwamo ya mikoa ya Arusha, Lindi, Mtwara Iringa na maeneo mengine nchini.
“Katika mashirika ambayo Ofisi Msajili wa Hazina tunayafurahia katika utendaji wao ni National Housing Corporation (NHC), kwamba bado imekuwa na utendaji mzuri na mageuzi ambayo wamekuwa wakiyafanya,” anasema Msajili wa Hazina, Mchechu.
Msajili wa Hazina ametaja mambo manne aliyosema ndio ujumbe wa ofisi yake kwa NHC akisema; “Ujumbe wetu mkubwa kwa NHC, la kwanza nikuendelea kuongeza kiwango cha uchangiaji.
Ni kwa sababu tunatamani mwakani au hata wakiweza mwaka huu, kiwango chao kifikie Sh bilioni 10. Kwa hiyo kwenye bajeti yao wanayokwenda kuweka tunahitaji kuona gawio la Serikali lifikie hivyo na tunaamili hilo litafanyika.”
Katika agizo lake la pili Mchechu anasema: “Tunaigiza NHC waangalie kasi ya uendeshaji miradi yao, iende ikaongezeke. Wana kasi nzuri, lakini tuna changamoto kubwa ya nyumba ndani ya nchi yetu. Kwa hiyo tunapozungumzia juu ya ujenzi wa nyumba lazima ufuate kama upo kwenye dharura.
Wawe kama kwenye chumba cha vita, ukienda kwa utaratibu wa kawaida unaokutaka tu utengeneze faida, hatutawawezesha Watanzania wengi kumiliki nyumba, tunataka kasi ya NHC iongezeke, wajipambanue ili wawe sehemu muhimu ya suluhisho la uhaba mkubwa wa nyumba tulionao.”
Msajili wa Hazina ametaja agizo la tatu kwa NHC kuwa ni kuwa na timu ambayo ina upendo, ina umoja ina mshikamano. Anasema hata kama NHC ingekuwa na watu wazuri kiasi gani, lakini kama hakuna upendo,hakuna mshikamano hawataweza kuwa na mafanikio mazuri.
"Wasia wangu mkubwa ni kwamba watu wanaofanya kazi pamoja, wawe na ubunifu, kusiwe na majungu kwa sababu, sisi huku serikalini hatutaki kuona watu wenye majungu au kusikia wanapigana majungu, tunataka akili hiyo ya kupika kajungu ikatumike katika ubunifu, utendaji kazi na kuboresha,”anasema Mchechu huku akiongeza;
“NHC ndiyo tegemeo la kumfanya mtanzania yoyote aweze kuishi katikati ya mji. Leo Mtanzaniayeyote ambaye hakuwahi kuishi upanga, tegemeo la pekee ni NHC kupitia nyumba zake.”
Katika agizo lake la nne, Msajili wa Hazina, Mchechu anasema ni muhimu kwa NHC kuangalia ni jinsi shirika hilo litakavyotumia ubunifu nakutumia rasilimali ilizonazo kuongeza kipato.
“La mwisho kati ya mengi ambalo tumetaka waliangalie ni jinsi gani NHC itatumia ubunifu kutekeleza vizuri miradi yake na pesa ili Kwenda kutekeleza miradi mingine. Mfano; NHC imeenda vizuri katika miradi ya ubia, wametuambia awamu ya pili ni miradi 61.
Tunatamani iendelee kwa kasi kubwa zaidi kwani hii inawapa asilimia 60 ya thamani ya nyumba ndani ya miaka15. NHC inafanya vizuri, lakini waendelee na mageuzi kupata mafanilio makubwa zaidi,” amesisitiza Msajili wa Hazina, Mchechu.
Awali, akitoa taarifa ya utekelezaji katika mwaka mmoja uliopita, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah amesisitiza umuhimu wa ushirikiano endelevu kati ya shirika hilo na na wadau wake katika kufanikisha malengo yake, huku akieleza namna wanavyotekeleza dira ya Msajili wa Hazina katika kukuza mapato.
Akizungumzia matengenezo na ongezeko la mapato, Hamad anasema matengenezo ya majengo yamefanyika nchi nzima, akieleza kwamba kutokana na maboresho hayo, mapato ya kodi yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 8.5 kwa mwezi (2023/24) hadi Shilingi bilioni 10 kwa mwezi (2024/25).
Kuhusu utekelezaji wa Miradi ya Faida ya Haraka (Quick Wins Projects),mkurugenzi huyo wa NHC amesema miradi hiyo inatekelezwa katika maeneo muhimu ikiwamo Masasi, Mtanda-Lindi, Kashozi-Bukoba, Zongomela-Kahama, na Tabora ili kuongeza mapato na thamani ya mali za NHC.
Ukusanyaji wa Madeni
Kuhusu madeni, Hamad anasema kwa sasa yamepungua kutoka Shilingi bilioni 27 (2023/24) hadi Shilingi bilioni 23 (2024/25)nakuaninisha hiyo imetokana na juhudi madhubuti za ufuatiliaji wa madeni.
Sera ya Ubia
Kuhusu eneo la ubia, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, anasema jumla ya miradi 20 yenye thamani ya Shilingi bilioni 279 inatekelezwa, huku miradi mingine 61 yenye thamani ya Shilingi bilioni 607.2 ikiendelea, NHC ikitarajiwa kuongeza eneo la ujenzi la mita za mraba 394,756.72.
Gawio la Serikali
Akizungumza kuhusu mapato ya NHC, Hamad anasema kutokana na ongezeko la mapato ya shirika hilo, gawio kwa Serikali limeongezeka kutoka Shilingi Shilingi bilioni 1.2 (2023/24)
“Naiomba Ofisi ya Msajili wa Hazina kusaidia katika urejeshaji wa madeni sugu kwa wateja wa NHC, lakini pia kuendelea kusaidia shirika kupata rasilimali zinazotokana na mabadiliko yanayoendelea katika mashirika ya umma ili kuimarisha mtaji wake,” anasema Hamad.
Amesisitiza kuwa NHC litaendelea kusimamia weledi, uadilifu na bidii, ili kuongeza ufanisi na kuendelea kuboresha maisha ya Watanzania.
Akifunga mkutano hadi kufikia Shilingi bilioni 6.5 (2024/25), huo wa Mwaka wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,
Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Dk. Sophia Kongela, licha ya kuwapongeza wajumbe kwa kujadili kwa umakini na kina zaidi bajeti ya mwaka 2025/26, amesisitiza bajeti hiyo ikahakikishe miradi ya ujenzi na ukarabati inatekelezwa kwa kasi zaidi.
0 Maoni