Tuzo za Utalii na Uhifadhi kuzinduliwa Disemba 20

 Na Hussein Ndubikile,daimatznews@gmail.com 

Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kukuza ba kuitangaza sekta ya utali ndani na nje ya nchi.
Dk Hassan Abbas
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Hassan Abbas amesema hayo leo Desemba 10,2024, wakati akitangaza kufanyika kwa Uzinduzi wa Tuzo ya Utalii na Uhifadhi utakaofanyika Disemba 20 mwaka huu jijini Arusha.

Dk. Abbas amesema Tanzania kwa mara ya kwanza itatoa tuzo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii wanakumbukwa kwa kutoa mchango ulioiwezesha sekta hiyo kupata mafanikio makubwa.

Katika hatua nyingine, Dk Hassan Abbas amezungumzia tuzo ambazo taifa imezipata dunianí na afrika kiujumla akieleza kuwa  zimetokana na Tanzania kuwa na vivutio bora, ambavyo vimekuwa vikichangia pato la taifa.
 
Dk. Abbas ametolea mfano wa maeneo hayo kuwa ni mbuga za wanyama za Serengeti, Ruaha, Ngorongoro pamoja na kuwepo na makumbusho ya kale ni miongoni mwa maeneo yanayochangia  kuingiza watalii wengi nchini

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi