Dubai, TCCIA zatia saini makubaliano kibiashara

-Yalenga kuimarisha biashara
-Biashara Dubai, Dar yafikia Dola bilioni 2.7 

Hussein Nubikile, daimatznews@gmail.com

Dubai International Chamber imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) ili kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji wa pande hizo mbili.
 Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chambers, Mohammad Ali Rashed Lootah (kulia) na rais waTCCIA, Vincent  Minja, wakitia saini makubaliano ya kibiashara Jijini Dar es Salaam, leo Desemba 12,2024.

.

Makubaliano hayo yametiwa saini leo Desemba 12,2024, katika Kongamano la Biashara “Kufanya Biashara na Tanzania” lililoandaliwa na Dubai International Chamber kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali, ikiwemo Ubalozi wa UAE na Tanzania, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

Makubaliano hayo yamesainiwa na Mohammad Ali Rashed Lootah, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chambers na Vincent Bruno Minja, Rais wa Chamber ya Tanzania (TCCIA) kwa niaba ya taasisi zao.

Kwa mujibu wa taasisi hizo, makubaliano hayo yametokana na juhudi za pande zote kuimarisha uhusiano kati ya kampuni za Dubai na Tanzania kwa kuandaa mipango ya kibiashara, mikutano na matukio ya biashara na kwamba pande hizo zitashirikiana maarifa, kubadilishana taarifa, na kuchunguza fursa za uwekezaji.

Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa TCCIA, Vincent  Minja amesema yatasaidia thamani ya Biashara na Uwekezaji kukuwa kwa haraka Tanzania.

Minja amesema kuwa kutokana na ushirikiano wa pande hizo thamani ya biashara isiyohusisha mafuta kati ya Tanzania na Dubai ilikua kwa asilimia 9 katika mwaka 2023na kufikia Dola za Kimarekani bilioni 2.7.
 
"Hadi kufikia mwisho wa Septemba 2024, jumla ya kampuni 274 kutoka Tanzania zimesajiliwa kama wanachama wa Dubai Chamber of Commerce, "amesema..

Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo wamesisitiza umuhimu wa kujenga madaraja ya kibiashara na kubainisha sekta zinazozalisha fursa kubwa za ushirikiano, ikiwamo kilimo, utalii, nishati na teknolojia zilizo na fursa kubwa Tanzania.

Sambamba na hayo amehimiza makampuni ya Kitanzania kuchangamkia fursa zilizopo Dubai, ikiwemo sekta ya Nishati na madini, Dawa na vifaa tiba, Kilimo, Uzalishaji viwandani na uendelezaji wa miundombinu na teknolojia

Hata hivyo TCCIA imejizatiti kuwa jukwaa la biashara kati ya Tanzania na Dubai, ikilenga kukuza ushirikiano wa kimkakati na kuhamasisha ukuaji wa kiuchumi kwa pande zote.Dubai International Chamber imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) ili kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji wa pande mbili.

Makubaliano hayo yalitiwa saini katika Kongamano la Biashara “Kufanya Biashara na Tanzania” lililoandaliwa na Dubai International Chamber kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali, ikiwemo Ubalozi wa UAE na Tanzania, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

Makubaliano hayo yamesainiwa Leo Jijini Dar es Salaam na Mohammad Ali Rashed Lootah, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chambers na Vincent Bruno Minja, Rais wa Chamber ya Tanzania (TCCIA).

Makubaliano hayo yanatokana na juhudi za pande zote kuimarisha uhusiano kati ya makampuni ya Dubai na Tanzania kwa kuandaa misheni za kibiashara, mikutano, na matukio ya biashara. Vilevile, pande hizi zitashirikiana maarifa, kubadilishana taarifa, na kuchunguza fursa za uwekezaji.

Aidha Mwenyekiti wa Chamber ya Tanzania TCCIA Bw. Minja amesema Makubaliano hayo yatasaidia thamani ya Biashara na Uwekezaji Kukuwa kwa Haraka Tanzania

Aidha thamani ya biashara isiyohusisha mafuta kati ya Tanzania na Dubai ilikua kwa 9% mwaka 2023, ikifikia Dola za Kimarekani bilioni 2.7. Hadi kufikia mwisho wa Septemba 2024, jumla ya makampuni 274 kutoka Tanzania yamesajiliwa kama wanachama wa Dubai Chamber of Commerce.

Hata hivyo Kongamano hilo limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali ambapo wamesisitiza umuhimu wa kujenga madaraja ya kibiashara na kubainisha sekta zinazozalisha fursa kubwa za ushirikiano, kama vile kilimo, utalii, nishati, na teknolojia ambazo ndio zenye fursa kubwa Tanzania.

Amehimiza kampuni za Kitanzania kuchangamkia fursa zilizopo Dubai katika sekta ya nishati na madini, dawa na vifaa tiba, kilimo, uzalishaji viwandani na uendelezaji wa miundombinu na teknolojia.

TCCIA imesema imejidhatiti kuwa jukwaa la biashara kati ya Tanzania na Dubai, ikilenga kukuza ushirikiano wa kimkakati na kuhamasisha ukuaji wa kiuchumi kwa pande zote.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi