-Yaishukuru kuondoa VAT nyumba za Sh50 mil
Exuperius Kachenje
Wakati uhaba wa nyumba za makazi ukielezwa kufikia nyumba 3,000 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeiomba Serikali kufikiria kuanzisha dirishala mikopo nafuu ya nyumba kwenye mabenki, ili kuwawezesha wananchi mmoja mmoja kuweza kukopa na kumiliki nyumba.
NHC pia imeomba Serikali kuwaondolea Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT), wananchi mmoja mmoja wanaonunua nyumba za shirika
hilo zenye thamani ya zaidi ya Sh50 milioni, huku wakiishukuru kwa kuanza kuchukua hatua kutokananakuondoa VAT kwa nyumba za shirika hilo zenye bei ya hadi Sh50 milioni.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Hamad Abdallah
ameota maombi hayo wakati akizungumza na wabunge wa Kamati ya Bunge ya
Uwekezaji na Mitaji ya Serikali (PIC), waliofanya ziara katika majengo nane yanayojengwa na NHC
kwenye Mji wa Serikali Ntumba mjini Dodoma Oktoba 26,2024.
“Tunaona Serikali imeweka Dirisha Maalum la
Mikopo ya Kilimo kwenye mabenki, tunaona kuna umuhimu pia Serikli likaanzisha
dirisha kama hilo kuwawezesha wananchi mmoja mmoja kupata mikopo nafuu yenye riba
ndogo kwa ajili ya kununua nyumba,” amesema Hamad na kuongeza:
“Tunadhani sekta ya nyumba iangaliwe kwa
mikopo zaidi yenye riba nafuu kupitia benki kwenda kwa wananchi."
Mkurugenzi Mkuu huyo wa NHC ameeleza hatua
hiyo itasaiia kupunguza tatizo la makazi na Watanzania wengi zaidi ikuweza
kumiliki nyumba hali itayosaidia pia kuboresha maisha ya wananchi na maendeleo kwa
ujumla.
“Tunadhani ni muhimu nyumba zinazouzwa na NHC ziondolewe Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT), katika ujenzi wake NHC ilishalipa VAT, wanunuzi wengi hulipa NHC kupitia benki hivyo hulipia tena na VAT, kimsingi mlaji wa mwisho tunadhani asilipe VAT, ila kwa kampuni zinazonunua nyumba VAT ibaki,” amesema Hamad.
![]() |
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC), Augustine Vuma (katikati) akizungumzana wanahabari baada ya kamati hiyo kutembelea miradi ya ujenzi wa ofisi za kudumu za wizara nane za Serikali wenye thamani ya Sh. bilioni 186.8 katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, Oktoba 26,2024. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, (Picha na Exuperius Kachenje) |
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeingia mikataba na Wizara Nane (8) ili kujenga ofisi za kudumu kwenye awamu ya pili katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, wenye thamani ya shilingi bilioni 186.8 yote yakiwa yamekamilika kwa wastani wa asilimia 87.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, NHC inajenga
majengo ya Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Wizara ya Madini, Wizara ya
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wizara ya Nishati.
Nyingine ni Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Pamoja
na Wizara ya Viwanda na Biashara.
0 Maoni