-Yatajwa pekee kwa Tanzania
Exuperius Kachenje, daimatznews@gmail.com
CRDB imetajwa kuwa benki bora zaidi nchini, iking'ara Afrika Mashariki na kutajwa miongoni mwa benki bora barani Afrika mwaka 2024.
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela |
Kwa mujibu wa Mtandao wa Kimataifa
Global News, Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF), zimeitaja
CRDB pia kuwa miongoni mwa benki bora duniani kwa mwaka huu 2024 ukanda wa Afrika.
Kwa mujibu wa mtandao huo uliochapisha habari hizo mapema mwezi huu Mei,2024,
kulichoipaisha CRDB kuingia kwenye benki ubora ni uwekezaji wake endelevu wa
dola milioni 300 (Tsh 780, bilioni) katika eneo uhifadhi mazingira, kupitia
mpango wake wa Kijani Bond.
Kwa ukanda wa Afrika Mashariki,
nchini Uganda Centenary Bank imetajwa kuwa mshindi wa ubora, wakati ambapo
imeadhimisha mika 40 mwaka uliopita 2023 ikiwa na wateja milioni 2.4 huku
ikikua kwa kasi.
Kwa mwaka huu, mshindi kutoka
nchini Kenya ni Co-operative Bank, inayotajwa kuwa na ongezeko kubwa la
mawakala, mtandao wake ukifikia mawakala 17,000 na kutajwa kuwa na asilimia 91 ya miamala kupitia
mfumo wa kidijitali.
Benki hizo tatu za Afrika
Mashariki, CRDB, Centenary na Cooperative, zimo miongoni mwa benki 35 bora
zilizoainishwa kwa Bara la Afrika na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha
Duniani.
0 Maoni