-Aendelea kuaminiwa kuitumikia CCM
Exuperius Kachenje, daimanewstz@gmail.com
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, amerejea madarakani kwa namna nyingine, safari hii akiteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Uteuzi wa Chongolo umefanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan leo na kutangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Dk. Moses Kusiluka.
Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi, umetaja pia wateule wengine na ukuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, sanjari na uhamisho wa watendaji wa nafasi hizo.
Chongolo anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe kutoka nafasi ya ukatibu mkuu wa CCM, aliyojiuzulu Novemb mwaka 2023 kwa kilichoelezwa ni kutokana na kuchafuliwa mtandaoni, jambo ambalo Rais Samia alisema linachunguzwa.
Hata hivyo, uteuzi huo unaweza kuelezwa kwamba Rais amejiridhisha na usafi wa Chongolo, ambaye alibeba jukumu la kuwajibika baada ya kuchafuliwa.
Unaweza kuelezwa pia ni wa kimkakati, utakaomfanya Chongolo aendelee kuitumikia CCM, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe akimwakilisha Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan.
Ikumbukwe kuwa nafasi ya ukatibu mkuu wa CCM imechukuliwa na Balozi Emanuel Nchimbi, huku Chongolo akichukua nafasi ya Dk.Francis Michael.
Zaidi, soma orodha ya wateule wapya na wanaohamishwa hapa chini.
0 Maoni