Makuburi Ally
CHAMA cha ACT Wazalendo kinatarajia kuwakutanisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwamo nia ya chama hicho kujitoa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (GNU).
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema hayo leo Machi 8,2024 mbele ya waandishi wa habari akieleza kwamba hatua hiyo ni zao la kikao cha Halmashauri Kuu Taifa ya ACT Wazalendo iliyokutana Machi 4 mwaka huu, makao makuu ya chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Amesema uwepo wa GNU ni utulivu wa kiuchumi, utalii, mikopo, biashara na kwamba roho ya uchumi wa Zanzibar inategemea utulivu.
"Kikao cha Halmashauri Kuu Taifa kilifanya tafakuri ya kina juu ya mwenendo na mwelekeo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar," amesema Shaibu.
Amebainisha kuwa Serikali hiyo ni matakwa kisheria kwa hoja tatu ambazo ni kuachiwa huru kwa viongozi wote wa ACT walioshikiliwa, watuhumiwa hao ni lazima wafidiwe sambamba na mageuzi ya kimfumo na usimamizi wa uchaguzi.
Mwisho
0 Maoni