Hot Posts

6/recent/ticker-posts


 Makamu wa Rais ahutubia UN 

Mwandishi Wetu, DAIMATANZANIA

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango, ameshiriki na kuhutubia mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaondelea katika Jiji la New York nchini Marekani, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango anaongoza ujumbe wa Tanzania ambapo awali Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa ulijadili kuhusu Malengo Endelevu 17 ya Dunia (SDGs), unaotarajiwa kufanyika Septemba 18 na 19, huku Tanzania ikitajwa kufanya vizuri.

Mkutano huo, umefanyika huku ripoti ya tathmini ya pili ya hiari iliyofanywa na Umoja wa Mataifa (UN) kati ya mwaka 2019 hadi Juni mwaka 2023, kuhusu utekelezaji malengo hayo kufikia mwaka 2030 (VNR) ikionyesha kuwa Tanzania imefanya vizuri katika maeneo sita.

Akiwasilisha mada katika kikao kazi na Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF), kwenye Ofisi za Shirika la Mpango wa Maendeleo Duniani (UNDP) leo jijini Dar es Salaam, mtaalam w uchumi kutoka ofisi hiyo, Evance Siangicha amebainisha kuwa Tanzania imefanya vizuri katika maeneo sita.

“Katika SDG 7: kuna mafanikio ya ongezeko la upatikanaji nishati ya kutosha. Idadi ya wananchi wanaotumia umeme imeongezeka kutoka asilimia 57.5 mwaka 2018 hadi asilimia 78.4 mwaka 2021. Kwa SDG 6:kuna ongezeko la upatikanaji wa maji safi hasa vijijini kutoka asilimia  70.1 mwaka 2019 hadi asilimia 74.5 mwaka 2021,” amesema Siangicha.

Ametaja maeneo mengine kuwa ni katika lengo namba SDG 2: akieleza  Tanzania inamaendeleo makubwa kuelekea kujiimarisha katika mifumo ya kujitosheleza kwa chakula kufikia mwaka 2030, huku ikipinguza upungufu wa chakula kutoka asilima 118 mwaka 2019 hadi asilimia 114 mwaka 2022 na kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

Kwa mujibu wa mchumi huyo kwenye SDG 9:Tanzania ina maendeleo mazuri katika kuimarisha miundombinu ya usafirishaji hasa reli ya kisasa, usafiri wa anga na barabara., ambapo pia imeimarisha mifumo ya taarifa za ardhi ikizindua na kupaisha mkakati wa kuwa na miji endelevu na jamii.

Awali katika mada yake, Ofisa mawasiliano kutoka UNDp, Usia Nkhoma-Ledama, amebainisha kuwa mkutano huo wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, utaongozwa na  Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Dennis Francis kutoka Trinidad & Tobago.


Chapisha Maoni

0 Maoni