MAELEKEZO YA RAIS DK. SAMIA MRADI UJENZI MATENKI YA MAFUTA HAYA HAPA
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amezipa maelekezo maalum wizara na taasisi za Serikali akizitaka kuhakikisha Mradi wa Ujenzi wa Matanki ya Kupokelea na Kuhifadhi Mafuta eneo la Kigamboni, Dar es Salaam unatekelezwa kwa wakati na kukidhi viwango vya kimataifa. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Matanki ya Kupokelea na Kuhifadhi Mafuta eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, Machi 3, 2026. Ameiagiza pia Wizara ya Nishati, kuhakikisha inaimarisha miundombinu ya hifadhi ya mafuta na taifa linakuwa na akiba ya kutosha, ili kukabiliana na misukosuko ya bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia, huku akieleza kwamba kupanda kwa bei ya mafuta duniani ni changamoto inayoongeza umuhimu wa kuwa na miundombinu madhubuti ya nishati. Rais Dk. Samia ametoa maelekezo hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo wa kimkakati, Machi 3, 2026, jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kwamba uwekezaji huo ni ha...