NHC yaomba Serikali ifikirie mikopo nafuu ya nyumba kwa wananchi

-Yaishukuru kuondoa VAT nyumba za Sh50 mil Exuperius Kachenje Wakati uhaba wa nyumba za makazi ukielezwa kufikia nyumba 3,000 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeiomba Serikali kufikiria kuanzisha dirishala mikopo nafuu ya nyumba kwenye mabenki, ili kuwawezesha wananchi mmoja mmoja kuweza kukopa na kumiliki nyumba. Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah (mbele), akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC), Augustine Vuma (nyuma yake) na wabunge wengine wa kamati hiyo kutembelea miradi ya ujenzi wa ofisi za kudumu za wizara nane za Serikali ulio na thamani ya Sh. bilioni 186.8 katika Mji wa SerikaliMtumba, Dodoma, Oktoba 26,2024 NHC pia imeomba Serikali kuwaondolea Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), wananchi mmoja mmoja wanaonunua nyumba za shirika hilo zenye thamani ya zaidi ya Sh50 milioni, huku wakiishukuru kwa kuanza kuchukua hatua kutokananakuondoa VAT kwa nyumba za shirika hilo zenye bei ya hadi Sh50 m...