Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2026

BEI MPYA KIKOMO YA PETROLI YAPAA

-Dar yauzwa Sh3,820 kutoka Sh2,864 mwezi Machi Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo ya mafuta ya petroli na dizeli zitakazoanza kutumika  leo Aprili Mosi,2026, huku bei ya chini ya petroli ikiwa Sh3,820 kwa lita na dizeli Sh3,806 jijini Dar es Salaam. Bei hiyo ina ongezeko la wastani wa Sh956 kwa petroli, huku dizeli ikiwa na ongezeko la Sh948, ikilinganishwa na bei ya bidhaa hiyo kwa mwezi Machi. Kwa mujibu EWURA, bei kikomo ya juu ya petroli ni Sh4,080 na dizeli Sh 4,066 Katoro mkoani Kagera, ambapo bei ya juu zaidi ya mafuta ya taa ni Sh3,945 Katoro, huku bei ya chini ni Sh3,684 kwa lita moja jijini Dar es Salaam. Mwezi uliopita wa Machi, bei kikomo ya chini kwa lita mafuta ya petroli ilikuwa Sh 2,864 kwa lita, huku dizeli ikiuzwa kwa Sh, 2,858 jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu EWURA, bei kikomo ya juu ya petroli kwa Machi ilikuwa ni Sh3,124 na dizeli Sh 3119 Katoro mkoani Kagera, ambapo bei ya juu zaidi ...