DAIMA TANZANIA

NINAWASALIMU katika jina la Mwenyezi Mungu wasomaji wote na wafuatiliaji wa habari kupitia mitandao ya kijamii popote mlipo ulimwenguni na kuwakaribisha katika mtandao huu mpya kabisa wa habari DAIMATANZANIA blogspot, Online Tv na Youtube chaneli. Ninayewakaribisha, jina langu ni Exuperius Kachenje , mwanzilishi na mmiliki wa mtanado huu, ambaye ni mwanahabari kwa zaidi ya miaka 25. E. KACHENJE Nimehudumu katika nafasi mbalimbali kwenye vyombo vya habari tofauti, kuanzia ngazi za chini hadi baraka ya kuongoza wengine kwa kuwa MPIGA PICHA MKUU, MHARIRI WA HABARI na MSANIFU MKUU WA KURASA. Baadhi ya maeneo niliyohudumi ni upigaji picha za habari, uandishi wa habari za michezo, habari za siasa, uchumi, jamii, afya, mazingira, utawala bora, habari za uchunguzi pamoja na makala mbalimbali. Vyombo vya habari nilivyowahi kuhudumia na nafasi nilizoshika ni pamoja na Magazeti ya Mfanyakazi (Mwandishi na Mpigapicha), Tafakari (Mwandishi na Mpigapicha Mkuu), Madaraka (Mwandishi na Mpig...