Bashungwa aahidi neema kwa wakandarasi wazawa
Na Selemani Msuya WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha mpango utakaowezesha wakandarasi wazawa kushiriki kwenye miradi mikubwa nchini. Waziri huyo pia ameeleza kukerwa kwake na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Wakandarasi (CRB), kushindwa kuwachukulia hatua kali wakandarasi wazembe. Aidha, Bashungwa amewashauri wahandisi hasa vijana kuunda kampuni za ukandarasi na ushauri ili waweze kutekeleza miradi mikubwa ya serikali kupitia Program ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT Ujenzi). Ameyasema hayo wakati wa Maadhimisho ya Miaka 21 ya Mpango wa Mafunzo kwa Wahandisi Wahitimu (SEAP), ambapo zaidi ya wahandisi 300 wamekula kiapo cha utii, baada ya kujengewa umahiri katika tasnia hiyo. Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwainua wahandisi na wakandarasi, hivyo chini ya uongozi wake anapambana kuhakikisha mpango wa kuwawezesha wazawa unakamilika kwa wakati. Waziri Bashungwa amesema ...